Friday, February 6, 2009

MAMBO YA WARSHA HAYOOOOO


Mafanikio niliyoyapata katika mafunzo ya kutumia mtandao kwa wanahabari nchini na hata duniani kote na umuhimu wake .
Mafunzo haya yamedumu kwa siku tano na kufadhiliwa na Taasisi ya vyombo vya Habari kusini mwa Afrika-MISA, chini ya mkufunzi bwana peik Johansson kutoka shirika la utangazaji la finland.

Katika warsha hii nimejifunza mambo mengi kikubwa zaidi ni namna ya kuweza kupata historia,kupata vyanzo mbalimbali vya habari kutoka sehemu mbalimbali dunia tena kwa njia rahisi tu kwa kutumia mtandao ambapo msomaji wako ni rahisi kuweza kusoma zaidi habari hiyo kwa kutumia viunganishi mbalimbali kwa mfano http://www.freemidia.com,www.dailynews.habari/ leo.com,www.raimwema.com ama http://www.ippmedia.com/ na nyingine nyingi kama hizo .
Kwa habari za mataifa mbalimbali mwandishi anapashwa pia kutumia mashirika mbalimbali ya habari ili kumuwezezsha msoji wake kuisoma habari hiyo kwa mitazamo tofauti katika mataifa kwa mfano mwandishi anaweza kutumia viunganishi vya www.bbc.co.uk,www.dwelle.com,http://www.bbc.co.uk,www.dwelle.com,http//www.reutars.com,www.aljazeera.com/om,www.aljazeera.com/ na http://www.cnn.com/ na mingine mingi ya aina hiyo.
Vivo hivyo hata katika kuandika habari za biashara na majanga mbalimbali lazima mwandishi awe na viunganishi vya habari hiyo ili kuwa na uwanja mpana wa kuelewa mambo na mitazamo tofauti kutoka kwa waandishi wengine.
Mambo mengine tulio jifunza ni matumizi ya mtandao ni namna ya kuweza kupata matamshi ya maneno kutoka lugha tofauti pamoja na kuweza kupata thamani ya pesa kutoka nchi moja kwenda nyingine kwa kutumia mtandao.
Cha msingi zaidi katika mafunzo haya tumejifunza kuwa ni mwiko kwa mwandishi kunakili kazi ya mwandishi mwenzake lakini anapaswa kusoma na kuelewa nini kimeandikwa nay eye atumie mawazo yake katika kuielemisha jamii.
USHAURI.
Ningependa mafunzo haya yatolewe pia kwa wanahabari walioko vijiji ili kuweza kuwa na mtandao mkubwa wa kupashana habari.

No comments:

Post a Comment